Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Majalis za Maombolezo ya Mwezi wa Muharram katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa International Foundation - Dar es Salaam, Tanzania zinaendelea kwa kila Siku, na Leo hii ilikuwa ni Sehemu ya Mfululizo wa Vikao hivyo vya Mwezi wa Muharram, ambapo mada muhimu imetolewa kuhusiana na: "Utambulisho wa John, Shahidi wa Karbala". Mada hii imebainishwa kupitia Khatibu wetu wa leo: Sheikh Abubakar Matulia na ametoa ufafanuzi wa kina zaidi kuhusiana na Maisha ya John, Sahaba wa Imam Hussein (as) aliyepigana vita vya Karbala sambamba na Mashahidi wa Karbala, akiwa ni mtu wa Jamii ya Kiafrika.

29 Juni 2025 - 20:16

Mfululizo wa Majlisi za Muharram Zinaendelea katika Chuo cha Al-Mustafa (s), Dar es Salaam | Mafunzo Kuhusu John, Sahaba Mtiifu wa Imam Hussein(as)

Kama tulivyodokeza hapo juu, katika Majlisi hii, Mzungumzaji: Sheikh Mtulia, alizungumzia maisha ya John, mmoja wa Mashahidi waaminifu wa Karbala, akaitaja asili yake, imani yake kwa Imam Hussein (a.s), na nafasi yake ya kipekee katika historia ya Ashura.

Mfululizo wa Majlisi za Muharram Zinaendelea katika Chuo cha Al-Mustafa (s), Dar es Salaam | Mafunzo Kuhusu John, Sahaba Mtiifu wa Imam Hussein(as)

Tukio hili ni sehemu ya mfululizo wa vikao vya maombolezo na mazingatio ya kimaadili katika Mwezi wa Muharram, kwa lengo la kujifunza kutoka kwa mafundisho ya Karbala na kuimarisha roho ya upambanaji kwa haki na uadilifu na kuitetea Misingi Sahihi ya Kiislamu kama walivyofanya Mashahidi wa Karbala wakiongozwa Sayyid wa Mashahidi - Imam Hussein (as).

Mfululizo wa Majlisi za Muharram Zinaendelea katika Chuo cha Al-Mustafa (s), Dar es Salaam | Mafunzo Kuhusu John, Sahaba Mtiifu wa Imam Hussein(as)

Mfululizo wa Majlisi za Muharram Zinaendelea katika Chuo cha Al-Mustafa (s), Dar es Salaam | Mafunzo Kuhusu John, Sahaba Mtiifu wa Imam Hussein(as)

Your Comment

You are replying to: .
captcha